Ripoti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali (IGAD) sasa inaonyesha kuwa watu milioni 42 katika nchi 6 wanachama huenda wakakabiliwa na uhaba wa chakula katika siku zijazo.
Kati ya idadi hiyo, zaidi ya watu milioni 1.8 katika maeneo kame na nusu kame nchini Kenya ni miongoni mwa walio katika hatari ya uhaba wa chakula.
Kenya inatarajiwa kupata mvua za chini ya wastani katika robo ya mwisho ya mwaka, hali inayoweza kusababisha uzalishaji mdogo wa mazao ya chakula, huku ripoti ya IGAD ikikadiria kuwa mvua kidogo nchini inaweza kuongeza idadi ya Wakenya walio katika hatari ya uhaba mkubwa wa chakula kutoka milioni 1.8 hadi milioni 2.1 ifikapo mwanzo wa 2026.
Launch of the IGAD Regional Focus of the 2025 Global Report on Food Crises https://t.co/IltAK6cFiW
— ICPAC (@IGAD_CPAC) September 16, 2025