BY ISAYA BURUGU 10TH OCT 2023- Mamia ya wakenya hivi leo wamekongamana katika ukumbi wa Bomas jijini Nairobi kusherehekea siku ya utamaduni ambayo ni sherehe ya kwanza ya aina yake iliyongozwa na mama taifa Bi Racheal Ruto

.

Wito wa wananchi kuungana ili kuendeleza taifa hili mbele ukitolewa na viongozi mbali mbali waliohudhuria hafla hiyo.Vyakula mbali mbali na mavazzi ya kiasilia yakionyeshwa kwa waliohudhuria.

 Kwa upande wake mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei aliyehudhuria hafla hiyo ameitisha kuwepo viongozi wanaochukukia ufisadi na kuitaka jamii kukatalia mbali ufisadi.Amesema juhudi zote ni sharti zielekezwe katika kuwafunzi vijana jinsi ya kujiepusha na ufisadi ili kujihakikishia taifa lisilo na ufisadi siku zijazo.

 

 Naye Waziri wa Utumishi wa Umma, Utendaji na Usimamizi wa Uwasilishaji Moses Kuria  anasema Kenya itaanza kufanyia biashara ujuzi wake wa kitamaduni na kufaidika nao

.Akizungumza katika ukumbi wa Bomas of Kenya wakati wa Siku ya Utamaduni Jumanne, Kuria alisema Kenya sasa inalindwa chini ya mkataba wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) 1970, kama ilivyotiwa saini na Kamati ya Michezo na Utamaduni ili kuhakikisha kuwa imeidhinishwa.

Kenya inaungana na nchi 39 za Kiafrika ambazo zimetia saini mkataba wa kutaka kukabiliana na biashara haramu ya vitu vya kale vya kitamaduni kwa kupiga marufuku uagizaji wao haramu, usafirishaji na uhamishaji wa umiliki. hekima ya mababu kutatua matatizo ya kisasa.Alitoa wito kwa Wakenya kutafakari kwa kina “tunatoka wapi kama taifa na tunakoenda kama watu.”.

October 10, 2023