Radio Osotua › Local News

Viongozi kaunti ya Mombasa waitaka serikali kuwahuzisha wenyeji katika swala la ubinafsishaji wa bandari

Local News October 10, 2023 Osotua

BY ISAYA BURUGU,10TH OCT,2023-Gavana wa Mombasa Abdiswamad Nasiri  amekariri wito wa ubinafsishwaji wa bandari ya Mombasa unaoendelezwa na serikali.Nasir anasema kile anachokataa ni kutowasisha wakaazi wa Mombasa.

Nasir ameyasema hayo katika hafla ya elimu katika kaunti ya Mombasa.Naye kinara wa Azimio la umoja Raila Odinga amepinga mchakato wa ubinafsishaji wa bandari ya Mombasa akitaka kaunti ya Mombasa kuwa washika dau katika mazungumzo hayo kama ilivyo kwenye bandari zingine za kimataifa.