BY ISAYA BURUGU,12TH NOV 2022-Wakfu wa KCB na shirika la kimaendeleo la ujerumani  hivi leo imesambaza vifaa 476 vya ujenzi  kwa vijana katika sekta ya ujenzi vinavyogharimu shilingi milioni 19 .

Hii ni kufuatia kukamilishwa kwa mafunzo ya kiufundi  kwenye baadhi ya taasisi zilizoidhinishwa kote nchini.Haya ni kulingana na ushirikiano kati ya mashirika hayo mawili  kwa lengo la kuongeza uwezo wa vijana hao kuajiriwa na kuwapa pato vijana 3500 katika sekta ya ujenzi.

Mpango  huo unatarajiwa kujaza pengo  lililoko kati ya vijana  wanaosaka ajira na  na ujuzi wa kiufundi unaozidi kuhitajika.Kuanzia mwaka ujao vijana wanaopata ujuzi kama huo kutoka kwa kundi hilo watapokea masharti rahisi kuanzisha biashar zao  chini ya mpango wa huduma za kibiashara wa wakfu wa KCB  hadi biashara zao zisimame.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo ,Mkurugenzi  wa  ushirikiano kwa benki ya KCB Esther Waititu amesema kuwa benki hiyo  inaendeshwa na  moyo wa kufanikisha biashara  kama njia moja ya kutoa suluhu  kwa changamoto zinazokumba jamii.

 

November 12, 2022