Mkuu wa Majeshi Robert Kibochi amewataka wanajeshi wa kenya kushirikiana vyema na wenzao wakati ambapo wanaelekea nchini DR Congo kwa oparesheni ya kulinda amani nchini humo.

Hatua hiyo inajiri wiki moja baada ya Rais William Ruto kuamuru kutumwa kwa wanajeshi 900 kutoka KDF kujiunga na ujumbe wa kulinda amani Kikosi cha Kanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga wanajeshi hao, Kibochi aliwahimiza waitumikie nchi hiyo kama vile wangeitumikia Kenya na kurejesha amani.Vilevile alisisitiza utaalam na tajriba kubwa ya jeshi la KDF na kuongeza kuwa wanajeshi hao wamehitimu kutekeleza jukumu hilo.

November 12, 2022