Waziri wa Afya Aden Duale ametangaza kukomeshwa kwa ada ya uanagenzi yaani attachment fee kwa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Matibabu cha Kenya (KMTC).

    Akizungumza katika Kongamano la 8 la Kisayansi la KMTC jijini Nairobi, Waziri huyo alisema ataanza na kufuta ada zinazotozwa katika hospitali za Level Six, zikiwemo Hospitali ya Kenyatta na Hospitali ya KU na zingine ambazo ziko chini ya wizara yake.

    CS Duale aliangazia tofauti katika ada za sasa, akitoa mifano ambapo baadhi ya hospitali hutoza Sh10,000, huku nyingine kama Kaunti ya Garissa hutoza Sh1,000, na nyingine Sh2,000.

    June 4, 2025