BY ISAYA BURUGU 24TH JULY,2024-Wanafunzi wa shule ya upili ya wavulana ya Kilgoris eneo la Trans mara magharibi kule Narok wanadaiwa kuteketeza bweni la shule lenye uwezo wa kuhifadhi wanafunzi wapatao 70 mwendo wa saa moja leo asubuhi.Mwalimu mkuu wa shule hiyo Philip Ole Limpaso Amedhibitisha kisa hicho huku akisema kwamba wanafunzi hao waliteketeza bweni hilo baada ya wao kupata kiamsha  kinywa na kwamba hakuna chochote  kilichoweza  kuokolewa. Limpaso kadhalika amedai kwamba wanafunzi hao walijaribu pia kuchoma darasa sawa na sehemu ya kula usiku lakini wakaweza kuzungumziwa na wakaenda kulala.

Mwalimu huyo mkuu amesema pia kwamba hakuna malalamishi yoyote ambayo wanafunzi hao wamewasilisha japo anasema jana jioni hawakuweza kupata maji kama kawaida baada ya transfoma yao kuharibika lakini walizungumza na maafisa wa kenya power walioahidi kufika leo kushughulikia tatizo hilo.

Mwalimu huyo aidha  ametoa wito kwa wanafunzi hao kuwa na mazoea ya kuzungumza kila mara shida yoyote inapotokea badala ya kuchukuwa sheria mikononi mwao na kuharibu mali.

Share the love
July 24, 2023