BY ISAYA BURUGU 24TH JULY 2023-Macho yote hivi leo yanaelekezwa katika mahakama kuu ya Kisii huku mahakama hiyo ikitarajiwa kutoa hukumu kuhusu kesi ambapo mtoto wa miaka mitatu alingolewa macho.

Watu watatu wakuu akiwemo pacifica nyakerario na Maina Ochogo waliopatikana na hatia watafahamu hatma yao.Mawakili wa upande wa mashataka na mtoto Sagini wamelezea matumaini yao kuwa hatimaye haki itatendeka na mtoto huyo kupata haki

.Kwa mjibu wa mawakili hao ni kwamba ni sharti mahakama itoe hukumu nzito kwa watuhumiwa kwani mtoto mchanga asiyekuwa na makosa aliyetembewa unyama huo.Hakimu mkaazi Christine Ogweno ndiye anayetoa hukumu hiyo.

 

 

 

 

 

 

Share the love
July 24, 2023