BY  ISAYA BURUGU 29TH DEC 2022-Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kundi la kigaidi la Alshabaab  wamewaua watu wawili kwa kuwapiga risasi mapema leo asubuhi  katika barabara  ya Lamu kuelekea Garsen katika kaunti ya Lamu.

Taarifa zinasema kuwa angalau wanamgambo 10  waliovalia sare za kijeshi  walikuwa wameweka kizuizi  kwenye barabara hiyo  na walikuwa wakiwauliza maswali wendesha magari  kabla ya maafisa wakijeshi kuwasii eneo hilo na makabiliano kuzuka.

Uvyatulianaji mkali wa risasi  kati ya wanamgambo hao na wanajeshi  ulizuka kabla yao kutorokea katika msitu  wa Boni. Maafisa hao walifanikiwa kuwaokoa watu wanne miongoni mwao raia wawili wa Italia waliokuwa wametekwa nyara na wanamgambo hao.

Miili ya watu waliouawa imepelekwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Mpeketoni huku polisi wakianzisha msako dhidi ya wanamgambo waliotoroka.

December 29, 2022