BY ISAYA BURUGU,29TH DEC 2022-Watu wawili wamepoteza  Maisha leo katika ajali ya barabarani  iliyohusisha lori na gari dogo aina ya pick up.

Ajali hiyo ilitokea kwenye barabara ya Kenol Muranga.

Kwa mjibu wa polisi ajali hiyo ya mwendo was aa nne za asubuhi ilitokea  baada ya dereva wa gari aina ya pick up  kujaribu kulipita matatu  moja kabla ya kugongana ana kwa ana na lori lililokuwa likija.

Dereva wa lori na taniboy wake walisunurika bila majeraha lakini watu wawili waliokuwa kwenye gairi aina ya pick up walifariki papo hapo.

Miili yao ilipelekwa kwenye hifadhi ya maiti ya General Kago mjini Thika  huku magari husika yakipelekwa katika kituo cha polisi cha Maragua.

 

 

 

December 29, 2022