BY ISAYA BURUGU,03,NOV,2022-Wanaume wawili wamefariki dunia baada ya kupigwa na umeme asubuhi ya leo huko Thika Kaunti ya Kiambu.

Kwa mjibu  wa duru  kutoka eneo hilo,wawili hao wanaripotiwa kukumbana na mauti yao walipokuwa wakiharibu milingoti ya taa za mtaani ili kuiba vifaa vya taa hizo.

Miili ya wanaume wawili waliofariki katika mtaa wa section 9 huko Thika asubuhi ya tarehe 3.Nov 2022/Picha /Hisani

 

Kisa hicho kimetokea katika eneo la section 9 mjini Thika.

Miili ya wawili hao imeondolea katika eneo la tukio na kupelekwa katika hifadhi ya miili ya general Kago huko Thika,uchunguzi ukianzishwa.

November 3, 2022