Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji ameiomba mahakama ya rufaa kukataa ombi la mbunge wa sirisia John Waluke la kuachiliwa kwa dhamana.

Mbunge huyo alikata rufaa baada ya kuhukumiwa kifungu cha miaka 67 gerezani kwa kosa la kuipunja bodi ya uhifadhi wa nafaka Zaidi ya shilingi milioni 300.

Nordin Haji ameitaka mahakama kutomwachilia mbunge huyo kwa bondi, baada ya mawakili wake kuelekea mahakamani kuitaka mahakama kumwachilia mbunge huyo kwa bondi huku kesi ya rufaa ikiendelea, wakisema kuwa mbunge huyo anafaa kuendelea na kuwatumikia wananchi wa eneobunge lake.

November 2, 2022