BY ISAYA BURUGU,2ND AUG,2023-Wito umetolewa kwa waseminari  kulinda miito yao kwa dhati kwani utukufu wa mungu huangaza kwa manabii wake.

Huu ndio ujumbe wa baba askofu wa jimbo katoliki la Ngong John Oballa Owaa katika hotuba yake kwa  waseminari wa jimbo hilo katika mkutano wao wa kila mwaka uliyoandaliwa leo katika kituo cha watakatifu wote senta mjini Ngong.

Askofu Oballa  amewaimiza waseminari kusimika neno la mungu katika mioyo yao na kufanya neno la mungu liwe dhamana inayoweza kubainika nje.

Baba askofu amewasisitizia waseminari hao umuhimu wa  kuwa watu wa kweli kuhusu miito yao na kujiepusha na kujifanya bandia kwaai siku moja wataanikwa hadharani  .

 

 

Share the love
August 2, 2023