Serikali imezindua awamu ya pili ya mpango wa ruzuku ya mbolea. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa awamu hiyo,Rais William Ruto alisema kuwa bei ya mbolea itapungua kutoka Ksh.3,500 hadi Ksh.2,500 kwa ghunia la kilo 50 katika awamu hii ya pili.

Hata hivyo rais Ruto alitoa wito kwa wakulima kuzidisha matumizi ya mbolea ili kuongeza uzalishaji wa kilimo nchini.

Kuhusiana na suala la kupanda kwa bei ya sukari nchini, rais Ruto ameeleza kuwa kupanda huko kumechangiwa na mkanganyiko na fujo katika sekta ya sukari sawa na ukosefu wa miwa ya kuvuna.

Share the love
August 2, 2023