Viongozi mbalimbali wa kisiasa pamoja na watangazaji wamemmiminia sifa tele mwendazake mtangazaji  mkongwe wa runinga Catherine Kasavuli.

Wakizungumza wakati wa hafla ya Ibaada ya wafu kwa mwendazake iliyoandaliwa katika kanisa la friends jijini Nairobi,marafiki na watu waliosoma naye wamemkumbuka Kasavuli kama mtu mchangamfu ,rafiki wa kweli na  mwanahabari mahiri.

Kinara wa chama cha Narc Kenya Martha Karua aliyehudhuria hafla hiyo, amemkumbuka Kasavuli kama mtu aliyekuwa rafiki wa wengi na ambaye hakumnyima usaidizi yeyote aliyemwendea kutaka msaada.

Kasavuli aliaga dunia juma moja lililopita baada ya kuugua saratani. Anatarajiwa kuzikwa jumamosi hii nyumbani kwao kaunti ya Vihiga.

January 12, 2023