BY ISAYA BURUGU,10TH DEC 2022-Watoto wawili wavulana wamejeruhiwa vibaya hivi leo baada kutegue kilipuzi cha kutekwa ardhini  walipokuw a wakilisha mbuzi wa baba yao katika Kijiji cha Kikurrukur  lokesheni ya  Majimoto kaunti hii ya Narok.

Wavulana hao wawili wa umri wa miaka  12  na miaka sita wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Narok  wakiwa hali mahututi   huku wakipata majeraha ya macho na miguuni.Taarifa kutoka eneo hilo   zimedokeza kuwa  kuna vilipuzi  na vifaa vingine  eneo hilo vilivyokuwa vikitumiwa kwa mazoezi ya kijeshi  miaka ya 1980.

Wenyeji wa eneo hilo wametakiwa kukaa mbali na vifaa vyovyote vya chuma  wanavyovishuku  na badala yake wapige ripoti kwa polisi haraka.

Maafisa kutoka kambi ya kijeshi ya wanahewa  iliyoko  karibu huko Narok Magharabi  wamearifiwa  na kutuma kikosi cha kulipua mabomu eneo hilo .

Tayari eneo hilo limezingirwa likisubiri watalamu wa mabomu.

 

 

 

 

 

December 10, 2022