BY ISAYA BURUGU ,12TH DEC 2022-Maafisa wa polisi eneo la Kilimani wamemtia mbaroni  jambazi sugu  anayeaminika kuwa kiongozi wa genge  ambalo limekuwa likijihusisha na visa vya wizi wa  kimabavu  eneo la kilimani na viungani mwake jijini Nairobi.

Peter Waithaka mwenye umri wa miaka 33 ametia mbaroni eneo la  Eastlands baada ya kuandamwa na makachero kw amuda wa saa 48.Katika ripot iliyotolewa na idara ya upepelezi wa jinai DCI, inadokeza kuwa Waithaka nanashukiwa kuwa ndie aliye tekeleza mauaji ya raia mmoja wa ugiriki Alex Marcopaulo, mnamo mwezi Oktoba.

Waithaka anasemekana kumwendea Marcopaulo  katika makutano ya barabara ya  Menellik-Ngong na watu wengnine wawili  na kumwibia bidhaa zake  na kumfyatulia risasi  na kumjeruhi upande wa kulia wa kifua chake kabla ya kutoroka kutumia pikipiki.

Baadaye  Marcopaulo aliaga dunia katika hospitali ya  Nairobi Women’s baada ya juhudi za kuokoa Maisha yake kutofanikiwa.DCI inasema Waithaka aliachiliwa hivi maajuzi kutoka jela baada ya kuhudumu miaka sita kwa kosa kama hilo.

 

 

December 12, 2022