BY ISAYA BURUGU 16TH AUG 2023-Watu sita wameuawa kwa kupigwa risasi katika kijiji cha Bula Tawakal eneo la Kunaso, Kaunti ya Garissa, kufuatia mapigano kati ya koo.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, marehemu hao waliripotiwa kuviziwa na kuuawa na watu wasiojulikana wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Probox.

Akithibitisha kisa hicho, Kamishna wa Kaunti ya Garissa John Otieno alisema shambulio hilo linashukiwa kuwa malipo baada ya mtu mwingine wa ukoo hasimu kuuawa pia.

Mkuu wa polisi alisema mshukiwa mmoja alikamatwa na anasaidia uchunguzi.

Aliongeza zaidi kuwa watu wasiopungua kumi kutoka kwa kila koo wameuawa katika mikasa ya koo inayosemekana kusababishwa na ugomvi wa muda mrefu wa ardhi.

August 16, 2023