Watu watatu wameshtakiwa kwa mauaji ya aliyekuwa mbunge wa Kasipul Charles Ong’odo Were. William Imoli Shigali almaarufu Imo, Edwin Oduor Odhiambo almaarufu Machuani na Ebel Ochieng almaarufu Dave Colo aidha wamekana hatia ya mauaji hayo.

    Watatu hao walishtakiwa baada ya mahakama kufahamishwa kuwa wako sawa kiakili kushtakiwa.Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani kufuatia agizo la awali la kuwataka kufanyiwa uchunguzi wa kiakili kabla ya kujibu mashataka.

    Kwa mujibu wa ripoti iliyowasilishwa mbele ya mahakama hiyo, wote watatu wamefanyiwa tathmini na kuruhusiwa na wataalamu wa afya, hivyo kufungua njia ya kuanza kwa kesi ya jinai.

    Hata hivyo, Upande wa mashtaka uliitaka mahakama kutowaachilia watatu hao kwa dhamana ikitaja wasiwasi mkubwa wa kiusalama.

    June 17, 2025

    Leave a Comment