Waziri wa Usalama wa Ndani nchini, Kithure Kindiki, amekiri rasmi kuwepo kwa tatizo kubwa la ufisadi na ubaguzi katika Idara ya Uhamiaji ya nchi.
Kauli hii imetolewa wakati wa kikao cha Kamati ya Utawala wa Kitaifa katika Bunge la Kitaifa. Waziri Kindiki ameonyesha dhamira ya kusafisha Idara ya Uhamiaji ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma za serikali unafanyika kwa ufanisi na kwa haraka bila kuingiliwa na vitendo vya ufisadi.
Katika mazungumzo yake mbele ya kamati, Waziri Kindiki alikiri kuwa zoezi la upatikanaji wa cheti cha Pasipoti limekuwa likikumbwa na changamoto kubwa, ikiwa ni pamoja na maafisa wa idara hiyo kudai rushwa ili kutoa huduma za pasipoti. Hata hivyo, aliahidi kuwa serikali itachukua hatua madhubuti kumaliza tatizo hili na kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika.
Kikao hicho pia waziri aliweka bayana mipango kabambe ya marekebisho katika Idara ya Trafiki kwa kushirikisha mamlaka za trafiki nchini. Lengo kuu la marekebisho haya ni kuboresha usalama barabarani na kupambana na uhalifu unaoshuhudiwa kwenye barabara za nchi nzima.
Waziri Kindiki alitangaza kuwa vizuizi vya barabarani vitaondolewa ifikapo mwezi Novemba na badala yake, maafisa wa kushika doria watahusihwa ili kusaidia katika kudumisha usalama wa barabarani.
https://twitter.com/KindikiKithure/status/1694698276853793054?s=20