BY ISAYA BURUGU 2TH AUG 2023-Wakazi wa  mji wa Narok  wamenufaika na msaada wa huduma za matibabu bila malipo  zilizotolewa katika uwanja wa Wiliam Ole Ntimama mjini Narok na shirika la AMREF kwa ushirikianolo na hospitali ya rufaa ya Narok saw ana wizara ya afya.Mshirikishi wa kijamii katika shirika la AMREF health Africa Eugine Muchai  amesema mpango huo unalenga kutoa huduma za uchunguzi wa magonjwa yasiyokuwa yakuambukizwa na kuwapa matibabu ya bure wenyeji.

Magonjwa yanayoshughulikiwa ni Pamoja na kisukari,shinikizo la danmu,aina mbali mbali za saratani na jinsi jamii na watu wengi wanakosa kuyatambua na viwnago vya magonjwa yenyewe.

Aidha amendelea kusema kuwa mpango huo unazingatia pia  kufanya uchunguzi wa ugonjwa wa HIV na ukimwi  Pamoja na kutoa chanja dhidi ya COVID19  na kupima.

Vile vile Muchai  kando na uchunguzi wa magonjw ahayo pia wanatoa huduma za ushauri  bure bila malipo  kuhusu mitindo yakimaisha, na jinsi mmoja anapaswa kuishi ikiwa ni Pamoja na lishe ili kujiepusha na magonjwa hayo.

 

 

August 25, 2023