Waziri wa elimu nchini Migos Ogamba amesema serikali ina mipango ya kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo vya Anuwai TVET hadi milioni mbili mwaka ujao.

    Waziri Migos akizungumza katika chuo cha kiufundi cha Maasai Mara vocational Training Centre eneo la Eor-Ekule Narok mashariki, ameeleza kuwa wanafunzi zaidi ya 1,500 wamejiunga na chuo hicho huku akisema kuwa serikali imeweka mipango ya kuhakikisha inafadhili elimu kwa wanafunzi wengi kwa vyuo hivyo vya kiufundi nchini.

    Waziri huyo aliongeza kuwa Serikali itaendelea kufanya uwekezaji wa kimkakati katika sekta ya TVET ili kuiweka upya kama lango la ujuzi na uwezeshaji wa vijana.

    September 3, 2025

    Leave a Comment