Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki anatarajiwa kuzuru eneo la Kerio Valley hii leo, kwa ziara ya ukaguzi wa operesheni ya usalama katika eneo hilo, kufuatia shambulizi la hivi majuzi la ujambazi lililosababisha vifo vya dada wawili katika eneo hilo.

Waziri kindiki ataongoza ujumbe wa usalama katika eneo hilo akitarajiwa pia kuongoza misururu ya mikutano na wakuu wa usalama, Pamoja na kuwahakikishia wenyeji usalama wao.

Hali ya taharuki imetanda katika eneo hilo, baada ya shambulizi lililotokea siku ya kwanza ya mwaka huu kusababisha viso vya dada hao ambao ni wanafunzi wa kidato cha 3 na darasa la 7 mtawalia. Mifugo wapatao 70 pia waliibiwa katika shambulizi hilo.

January 3, 2023