Mji wa pwani wa Brazil wa Santos, ambao gwiji wa michezo Pele alianzia kuchezea na kupata umaarufu wake, umekua ukiendeleza shughuli ya kutoa heshima zake za mwisho siku ya leo kwa shughuli inayotarajiwa kuendelea kwa kipindi cha saa 24.

Gwiji huyo wa soka aliaga dunia siku ya alhamisi juma lililopita akiwa na umri wa miaka 82, baada ya kuugua saratani ya utumbo mkubwa. Mwili wa Pele uliwasili chini ya fataki huko Santos mapema leo kutoka Hospitali ya Albert Einstein ya Sao Paulo.

Kumbukumbu itafanyika kwa Pele, katika uwanja wa Vila Belmiro, nyumbani kwa Klabu ya Soka ya Santos.

Siku ya Kesho, maandamano ya kubeba jeneza lake yatapita katika mitaa ya Santos, na kuishia katika makaburi ya Ecumenical Memorial Necropolis, ambapo atazikwa kwa shughuli ya faragha.

January 2, 2023