Moses Kuria

Waziri wa Utumishi wa Umma, Moses Kuria, ametoa ilani kali kwa maafisa wa umma wanaozembea katika utoaji wa huduma kwa wananchi. Taarifa hii imetolewa wakati wa kikao cha waandishi wa habari kilichofanyika baada yake kupokea nyaraka za ofisi hiyo kutoka kwa mtangulizi wake, Waziri Aisha Jumwa.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Kuria amesema kwamba maafisa wanaozembea kazini wataondolewa kutoka kwa nafasi zao ili kuwapa nafasi watu wenye uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Aidha ameeleza kuwa ni muhimu kwa maafisa wa umma kutoa huduma bora kwa wananchi na kuhakikisha kuwa serikali inatekeleza majukumu yake kwa njia inayofaa.

Waziri Kuria, ambaye awali alihudumu katika Wizara ya Biashara na Viwanda kabla ya uhamisho wake kwenda Wizara ya Utumishi wa Umma, pia ameapa kushirikiana na serikali za kaunti kuhakikisha kuwa maafisa wote wanaotatiza utoaji wa huduma kwa wananchi wanachukuliwa hatua zinazofaa kisheria.

October 16, 2023