Naibu wa rais rigathi Gachagua amezindua rasmi kongamano la afya la siku nne litakalowaleta pamoja wadau wa afya huku mpango wa Afya kwa wote UHC ukitarajiwa kuzinduliwa siku ya Maadhimisho ya Mashujaa tarehe 20 mwezi huu.

Akizungumza baada ya kuzindua kongamano hilo katika kaunti ya Kericho, Rigathi amesema kuwa hali mbaya ya kiafya inasababisha familia nyingi nchini kutumbukia katika umaskini kwani Wakenya wengi hawawezi kupata bima ya afya.

Ameongeza kuwa mpango wa UHC utahakikisha utoaji bora wa huduma za afya.

Kwa upande wake waziri wa afya Susan Nakhumicha, akizungumza katika kongamano hilo amedhibitisha kwamba wizara yake imekamilisha utoaji wa vifaa vya matibabu kwa kaunti zote humu nchini baada ya kuzinduliwa kwa zoezi hili na Rais William Ruto tarehe 25 mwezi jana.

 

October 16, 2023