Wizara ya Ulinzi nchini Kenya inaazimia kuimarisha uwezo wa taifa katika kujilinda dhidi ya vitisho vya mtandao kwa lengo la kuhakikisha usalama wa taifa na taarifa zake.

Hatua hii inajitokeza kutokana na matamshi ya Waziri wa Ulinzi, Bwana Aden Duale, ambaye amesisitiza umuhimu wa kulinda mifumo ya kidijitali ya nchi.

Akizungumza alipohudhuria kongamano la kwanza la Chuo Kikuu cha Ulinzi nchini, lililofanyika katika eneo la Lanet, Waziri Duale alisisitiza kwamba usalama wa mtandao ni msingi muhimu kwa maendeleo na ulinzi wa taifa. Aliongeza kuwa uwezo wa taifa kufanya shughuli zake bila kuingiliwa au kuhofia wizi wa taarifa muhimu kwenye mtandao unategemea sana usalama wa mifumo ya kidijitali.

Kongamano hilo pia lilihudhuriwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Bwana Eliud Owalo.

 

Share the love
October 26, 2023