Wafadhili watatu wa Kimarekani wanaofanya kazi na shirika la Child Refuge Centre International waliangamia katika ajali mbaya ya barabarani kwenye Barabara Kuu ya Narok-Maasai Mara karibu na uwanja wa ndege wa Ewaso nyiro.

Watatu hao ambao wamekuwa Narok Magharibi wakiendesha vituo vingine tisa nchini walikuwa wakielekea katika eneo la Sekenani ambapo gari lao liligongana ana kwa ana na trela lililokuwa likisafirisha mizigo.

Akithibitisha kisa hicho, OCPD wa Narok ya kati John Momanyi amesema kuwa mmoja wa raia hao wa kimarekani aliaga dunia papo hapo huku wawili wakiaga walipofikishwa hospitalini.

Kwa upande wake Alex Nkuruna mmoja wa wakaazi ambao wamekuwa wakinufaika na ufadhili wa mishonari hao ameelezea kusikitishwa kwake kufuatia vifo vya watatu hao.

October 26, 2023