Jumla ya wafanyakazi 7,414 wa Huduma ya Afya kwa Wote (UHC) wanatazamiwa kuajiriwa kwa masharti ya kudumu na ya pensheni kuanzia Septemba 2025.

    Haya yanajiri kufuatia zoezi la pamoja la kuhesabu wahudumu wa afya nchini kote lililofanywa na Idara ya Serikali ya Huduma za Matibabu kwa ushirikiano na Baraza la Magavana (CoG).

    Akihutubia wanahabari Jumatatu alasiri, Waziri wa Afya Aden Duale alifichua kuwa jumla ya madaktari 7,629 walithibitishwa. Hata hivyo, watu 215 ambao walishindwa kujiwasilisha walitambuliwa kama wafanyakazi hewa na mishahara yao ilisimamishwa, ikisubiri uchunguzi zaidi.

    August 25, 2025