Tume ya huduma kwa polisi NPSC imewatolea wakenya hakikisho kwamba zoezi la kuwachagua makurutu wapya wa polisi, itakuwa wazi, jumuishi na halitahusisha shuguli zozote za udanganyifu.

    Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya usalama katika bunge la kitaifa, afisa mkuu mtendaji wa tume ya NPSC Peter Leley, alisisitiza kwamba mikakati kabambe imewekwa na tume hiyo ili kuhakikisha usawa katika zoezi hilo ambalo pia litajumuisha watu kutoka jamii za wachache nchini.

    Leley alisema tume hiyo imeshirikisha wadau wakuu, akiwemo waziri wa usalama wa Ndani, ambaye mchango wake umeingizwa katika mfumo wa ugawaji wa zoezi hilo.

    NPSC inataka kuajiri askari 10,000 chini ya kanuni mpya iliyoundwa ili kukuza uwazi baada ya mazoezi ya hapo awali kugubikwa na malalamishi ya hongo na upendeleo.

    NPS inapania kujaza nafasi 10,000 ambapo kati ya idadi hiyo, nafasi 4,000 zimetengewa wahitimu wa NYS.

    September 9, 2025

    Leave a Comment