Wakaazi wa mpakani wameendelea kuwa na wasiwasi kutokana na uwezekano wa virusi vya ebola kuingia humu nchini.Wakizungumza na waandishi wa habari,wakaazi hao wamesema kuwa wana hofu ikizingatiwa kwamba baadhi ya wakaazi wa Uganda bado wanaingia nchini.Aidha naibu kaunti kamishna wa Busia Kipchumba Ruto amesema kuwa wameweka mikakati ya kutosha kudhibiti msambao wa virusi hivyo humu nchini.

Katika nchi jirani ya Uganda,wizara ya afya imedhibitisha kufariki kwa daktari mwingine kutokana na virusi vya ebola,idadi hii ikifisha kumi idadi jumla ya watu walioaga kutokana na virusi hivyo.Kifo cha daktari huyo kinajiri wiki moja tu baada ya rais wa taifa hilo Yoweri Museveni kusema kuwa hapana haja ya kuweka vikwazo vya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo ikizingatiwa kwamba virusi hivyo havisambai kwa kasi ikilinganishwa na virusi vya korona vinayosababisha ugonjwa wa covid-19.

October 5, 2022