By: Brigit Agwenge,

5th Oct 2022,

Siku chache tu baada ya mtoto wa rais wa Uganda Muhoozi Kainerugaba kuzua dhoruba kwa msururu wa ujumbe wa Twitter uliosababisha mgawanyiko baina ya kenya na taifa hilo, rais wa Uganda Yoweri Museveni ameomba msamaha kwa Rais wa Kenya William Ruto.

Museveni ameeleza kuwa si sahihi kwa maafisa wa Umma, wawe wa kiraia au wa kijeshi, kutoa maoni yao au kuingilia kwa njia yoyote mambo ya ndani ya nchi jirani.Aidha Museveni amemtetea mwanawe na kusema kuwa kosa hili ni kipengele kimoja ambapo ametenda vibaya kama afisa wa Umma hata hivyo, kuna michango mingine mingi mema ambayo Jenerali Muhoozi ametoa na bado anaweza kutoa. Itakumbukwa kwamba Kupitia mtandao wake wa twitter, Kainerugaba alisema itamchukua yeye na vikosi vyake wiki mbili tu kuivamia Kenya na kuuteka mji wa Nairobi.

October 5, 2022