BY ISAYA BURUGU.,02,NOV,2022-Mwanamme mmoja jijini Mombasa ameshtakiwa kwa kosa la kuwashambulia polisi wawili.Taarifa  zasema kuwa , polisi hao wawili walikuwa wanafanya doria katika sehemu ya Kibokoni wakati walikutana na mwanaume huyo na kutaka kumsaili wakati walipatana na harufu kali ya dawa ya kulevya aina ya bangi.

Badala ya kumfanyia usaili, mwanaume huyo kwa jina Salim Nasoro aliwageuzia polisi kibao na kuwashambulia kwa fimbo ambapo alimpiga mmoja miguuni na mwingine kwenye mmoja wa mkono wake. Walimuuliza kwa nini alikuwa akizurura na fimbo.

Mshukiwa huyo anadaiwa kuwa mkali na kuanza kuwachapa viboko maafisa hao mmoja baada ya mwingine. Lakini maafisa hao walimzidi nguvu mshukiwa, wakampiga mweleka chini na kumfunga pingu kabla ya kumsindikiza hadi Kituo Kikuu cha Polisi.Maafisa hao kisha walikwenda kwenye zahanati iliyokuwa karibu kwa matibabu na walipewa fomu za P3 (kwa ajili ya kuripoti shambulio hilo).Bw Nasoro alifika mbele ya Hakimu Mkuu wa Mombasa Martha Mutuku na kukana kutenda makosa hayo.

Aliachiliwa kwa bondi ya Sh 200,000 na mdhamini mmoja wa kiasi sawa na hicho au dhamana mbadala ya pesa taslimu Sh100,000. Kesi hiyo itatajwa Novemba 17.

November 2, 2022