BY ISAYA BURUGU,6TH MARCH,2023-Wito umetolewa kwa akina mama wajawazito katika eneo la Nkarone Samburu mashariki kutafuta huduma za afya hospitalini wanapokuwa wajawazito.

Hatua hiyo inalenga kupunguza visa vya  vifo vya akina mama wakati wakujifungua.

Kaunti ya Samburu imerekodi asiliami 18 ya visa vya akina mama kujifungua wakawai nyumbani.

Hata hivyo akina mama wajawazito katika kaunti hiyo wanataja safari ndefu wanazolazimika kutembea kusaka matibabu kama sababu kuu inayowafanya kusalia nyumbani na kutafuta huduma za wakunga.

March 6, 2023