Katibu mpya wa chama cha UDA Cleophas Malala, amependekeza vyama tanzu katika muungano huo kujiunga katika chama kimoja kabla ya uchaguzi wa mwaka 2027.

Malala ameeleza kwamba vyama vinavyounda muungano wa Kenya kwanza vinafaa kujiunga na chama cha UDA, kama mojawapo ya njia za kuonyesha uaminifu wao kwa rais William Ruto, huku akiorodhesha vyama vya CCM na ANC nchini Tanzania na Afrika Kusini kama baadhi ya mataifa yaliyofuata mkondo huu.

Baadhi ya vyama vinavyounda Kenya Kwanza ni pamoja na ANC ya Musalia Mudavadi, Ford Kenya ya Moses Wetangula na MCC ya Dkt Alfred Mutua, miongoni mwa vingine.

Kutwa ya leo, Malala aliongoza shughuli za uongozi wa Ofisi za chama cha UDA katika kauti ya Kisumu.

Share the love
March 4, 2023

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

%d bloggers like this: