Gavana wa kaunti hii ya Narok Patrick Ole Ntutu amezindua rasmi ujenzi wa chumba cha kujifungua katika zahanati ya Takitech ilioko eneo la Oloolmasani Transmara mashariki.

Ntutu ameeleza kuwa ujenzi huo umeanzishwa kufuatia ombi la wakaazi wa eneo hilo ambao wamekuwa wakihangaika kwa muda mrefu kutoka na ukosefu wa kituo hicho.

Ameongeza kuwa Utawala wake umeupa kipaumbele utoaji wa huduma za afya na hivyo watajenga vituo zaidi  katika zahanati za Njipiship, Kapweria, na Chesoen.

March 6, 2023