Watu kutoka pembe zote za dunia walikongamana hii leo katika chuo kikuu cha Maseno tawi la Yala kumpa mkono wa buriani aliyekuwa waziri wa Elimu Prof. George Magoha ambaye amezikwa nyumbani kwake katika kijiji cha Umiru.

Familia ya Magoha wakiongozwa na mkewe Barbara Magoha, walimmiminia sifa tele na kumtaja kama mtu ambaye alifanya kila awezalo kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Maafisa wa ngazi ya juu akiwemo aliyekuwa rais Uhuru Kenyatta walihudhuria hafla hiyo ya mazishi ya aliyekuwa Waziri wa elimu Profesa Gorege Magoha  katika kaunti ya Saiya.

Rais huyo wa zamani, alisema kuwa Magoha hakuangalia kabila, dini wala rangi alipokuwa waziri wa elimi ila alihakikisha kuwa wanafunzi wote wanatapata nafasi sawa katika sekta ya elimu.

Naye kinara wa upinzani Raila Odinga kwa upande wake amesema kuwa marehemu Prof. Magoha hakutapatapa kwenye maneno yake na kile alichokisema ndicho alisimama nacho.

Hata hivyo rais Wiliam Ruto hakuhudhuria hafla hiyo ila aliwakilishwa na waziri wa mawasiliano Eliud Owalo.

Magoha alifariki tarehe 24 mwezi jana katika hopsitali ya Nairobi baada ya kukumbwa na mshtuko wa moyo.

February 11, 2023