Asilimia 62% ya Wakenya wanaamini kuwa nchi inaelekea pabaya kulingana na utafiti uliofanywa na shirika la InfoTrak.

Katika ripoti hiyo iliyotolewa Jumanne, idadi kubwa ya Wakenya walihusisha madai yao na masuala muhimu yanayokabili taifa ikiwemo gharama ya juu ya maisha, ushuru na viwango vya juu vya ukosefu wa ajira.

Wengine walitaja utawala mbovu kuanzia kwa viongozi, siasa mbovu, majanga yakiwemo ukame na umaskini. Aidha asilimia 22 ya Wakenya wanaamini kuwa taifa linaelekea pazuri kwani kuna amani na utangamano.

 Kuhusiana na suala la utendakazi wa mawaziri humu nchini, waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki na mwenzake wa elimu Ezekiel Machogu wameorodheshwa kama mawaziri waliotekeleza kazi zao vyema ndani siku 100 ofisini.

February 28, 2023