Askofu mkuu wa jimbo kuu la Kisumu Maurice Muhatia Makumba ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la maaskofu wa kanisa katoliki KCCB kwa muda wa miaka tatu ijayo.

Askofu mkuu Muhatia, anachukua nafasi hii kutoka kwa Askofu mkuu wa jimbo kuu la Mombasa Martin Kivuva ambaye amekamilisha atamu yake ya miaka mitatu.

Viongozi wengine wapya walioteuliwa kwenye baraza hilo ni Askofu mkuu wa jimbo kuu la Nyeri Anthony Muheria ambaye atahudumu kama naibu mwenyekiti wa baraza hilo.

April 11, 2024