BY ISAYA BURUGU 29TH NOV 2022-Askofu wa jimbo katoliki la Ngong John Oballa Owaa hivi leo ameongoza misa ya mazishi kwa Mwenda zake mkewe mzee Paul Ndumia Mary Ndumia Wambui.Misa hiyo imeandaliwa katika parokia ya mtakatifu Paulo karangia.Wakati wa  ibada hiyo baba askofu amewahimiza wazazi kuwa katika mstari wa mbele kutoa mwelekeo unaofaa kwa Watoto wao ili kuwasaidia kufanya maamuzi muhimu haswa kuhusu maswala ya Imani akisema kuwa kumekuwa na ulegevu.

Misa hiyo imehudhuriwa  na mapadri na watawa  kutoka dekania mbali mbali akiwemo Edmund Tarimo ambaye ni baba paroko wa parokia ya mtakatifu petero mjini Narok.

Askofu Oballa pia amewataka waumini kuwajali wazazi na kusimama Pamoja nao kila wakati.Msimamizi wa makao makuu ya jimbo katoliki la ngo padri John nteseiyia pia amehudhuria ibada hiyo.

Mzee Ndumia ni shabiki sugu wa idhaa ya radio Osotua na pia ni mshiriki wa parokia ya mtakatifu Petro mjini Narok yanakopatikana makao makuu ya Radio Osotua.AMarehemu alifariki juma lililopita katika hospitali ya rufaa ya Narok ambako amekuwa akipokea matibabu.

 

 

 

 

 

 

November 29, 2022