Rais William Ruto amewaomba viongozi wa Upinzani kutafuta mbinu mbadala za kueleza kutoridhika kwao na jinsi serikali ya Kenya kwanza inatekeleza majukumu yake badala ya kuandaa maandamano.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kituo cha usambazaji cha Twiga, Rais ameweka wazi kuwa wanakubali kukosolewa na Upinzani ila amewataka kutowachochea wakenya dhidi ya wenzao na badala yake kutafuta mbinu mbadala za kuhakikisha kuwa sauti yao inasikika.

Na huku hayo yakijiri, muungano wa Azimio la Umoja umetangaza kuwa utaandaa mkutano wa wajumbe wa muungano huo hio kesho, ili kujadili maswala yanayosibu taifa la Kenya kwa sasa.

Kiongozi wa walio wachache katika bunge la kitaifa Opiyo wandayi ameeleza kuwa kikao cha kesho kitatumiwa na muungano huo kuweka mipango yao ya jinsi ya kusaidia katika kuyatetea maslahi ya wakenya.

November 28, 2022