Raila in Yatta

Kinara wa upinzani Raila Odinga amemtaka Rais William Ruto kupunguza gharama ya Maisha, na kupunguza mapendekezo yaliyo kwenye mswada wa fedha wa mwaka huu.

Akizungumza katika eneo la Yatta katika kikao cha muungano wa Azimio la Umoja, Odinga aliyeambatana na viongozi wengine wa muungano huo, amesema kwamba iwapo serikali itaendelea kuwadhalilisha wakenya, basi watalazimika kuchukua hatua zingine ili kukabiliana na mapendekezo ya serikali. Odinga aidha ameeleza kwamba sharti matakwa mengine waliyowasilisha hapo awali pia yaangaziwe.

Kwa upande wake, kinara wa Narc Kenya Martha Karua, ameeleza kusikitishwa na vita vinayoelekezwa kwa wafuasi wa muungano huo, akitaja kisa cha hivi karibuni cha kukamatwa kwa aliyekuwa kiongozi wa Kundi la Mungiki kama moja ya njia za kuwahangaisha wafuasi wa muungano wa Azimio.

 

May 26, 2023