Naibu Rais Rigathi Gachagua amemtaka Rais William Ruto kutozingatia wale wanaopinga asilimia 3 ya ushuru wa nyumba.

Akizungumza mjini Embu, Gachagua amesema wanaokosoa mradi huo kamwe hawatathamini ufanisi wa rais.

Alidokeza kuwa miradi hiyo ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu itakomesha ukuaji wa vitongoji duni nchini huku akitoa changamoto kwa wakosoaji hao kuja na mkakati bora zaidi wa kusaidia kupunguza ongezeko la vitongoji duni nchini.

Aidha alikariri kuwa mradi huo utabuni nafasi za ajira kwa vijana wasio na kazi nchini.

May 26, 2023