Kindiki

Waziri wa usalama wa ndaki Kithure kindiki ametuma onyo kali kwa wahubiri wengine wanaoendelea kuwapunja wakenya na kuwahangaisha huku wakijificha nyuma ya dini.

Akizungumza katika kikao cha bunge alipojiwasilisha ili kuhojiwa na wabunge kuhusu hali ya operesheni ya uokozi katika eneo la Shakahola.

Waziri Kindiki alieleza kwamba idara ya usalama haitasimamishwa na yeyote katika harakati za kuwakabili wahalifu wa aina hii, akisema kwamba muda wa kuwadhulumu wakenya kwa kisingizio cha dini umeisha.

May 26, 2023