By Isaya Burugu/DW,Oct 11,2022-Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeanza kujadili muswada wa azimio la kuitaka Urusi kuachana na mpango wake wa kuyanyakuwa majimbo manne ya Ukraine, mjadala ambao umetokea baada ya mfululizo wa mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine ambayo yamelaaniwa na nchi nyingi duniani.

Balozi wa Ukraine katika Umoja wa Mataifa Sergey Kysly-tsya amesema kwa kuyashambulia maeneo ya kiraia muda wa watoto kwenda mashuleni, Urusi imethibitisha kuwa ni taifa la kigaidi.

Urusi kwa upande wake imesema iliilenga miundombinu ya nishati na ya kijeshi, kulipiza kisasi ilichokiita shambulizi la kigaidi la Ukraine kwenye daraja la Kerch siku ya Jumamosi. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres pia alisema alishtushwa na mashambulizi ya Urusi ya Jumatatu. Mjadala huu utaendelea hadi kesho Jumatano na utahitimishwa na kulipigia kura azimio hilo.

October 11, 2022