BY  ISAYA BURUGU,11TH OCT,2022- Rais William Ruto amesema kuwa soko la hisa la Nairobi lina uwezo mkubwa kuisaidia nchi kutatua matatizo mengi yanayohusu fedha iwapo mikakati mwafaka itawekwa kuboresha utenda kazi wake.

Akizungumza alipofanya ziara kwa soko hilo na kuleta Pamoja wakurugenzi wa makampuni  mbali mbali nchini sawa  na usimamizi wa soko hilo la hisa,Ruto amesema kuwa serikali yake  imo mbioni kubuni mikakati kwa ushirikiano na kampuni za uzalishaji na uwekezaji itakayopelekea kunawiri kwa soko hilo.

Aidha rais amelezea haja iliyoko ya kuifanyia mageuzi sheria iliyoko ya ubinafsishwaji wa mashirika anayosema kwa sasa haina manufaa kwa taifa hili.

Vilevile rais amepiga kengele kiashirio cha uzinduzi wa mwamko mpya wa utenda kazi katika soko hilo.

October 11, 2022