By  Isaya Burugu,Oct 11,2022-Tume ya kitaifa ya huduma kwa polisi hivi leo inawahoji waliotuma maombi kujaza nafasi ya mkurugenzi mkuu wa idara ya upelelezi wa jinai DCI.

Hatua hiyo inafuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa mkurugenzi George Kinoti.Watu kumi wametuma maombi ya kujaza nafasi hiyo.

Mahoijiano hayo yanandaliwa katika chuo cha mafunzo ya serikali yaani Kenya school of government jijini Nairobi.

October 11, 2022