Zaidi ya bunduki 140 zilizokuwa zikimilikiwa kinyume cha sheria na raia wa maeneo la Kaskazini mwa bonde la Ufa, zimerejeshwa kwa maafisa wa usalama kufikia sasa.
Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki aidha ametoa onyo kuwa muda wa kurejesha silaha hizo hautaongezwa, huku awamu ya pili ya operesheni ya kurejesha utulivu katika maeneo hayo ikitarajiwa kutangazwa rasmi hio kesho.
Katika taarifa yake kwa taifa alasiri ya leo, Waziri Kindiki ameeleza kwamba wizara yake italikomboa eneo hilo kutoka kwa minyororo ya majambazi hawa.
https://twitter.com/KindikiKithure/status/1633824912732479489?s=20
Aidha Kindiki amelaani hatua ya viongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja, kwa kujaribu kuhitilafiana na shughuli za uchunguzi wa idara ya DCI, hasa baada ya mkwaruzano ulioshuhudiwa katika ofisi za DCI wakati sehemu ya viongozi wa muungano huo wakiongozwa na Raila Odinga walikita kambi katika lango kuu la makao hayo.
Waziri Kindiki ameeleza kwamba hali ya kuwahangaisha maafisa walio kazini haitakubali kwa vyovyote vile.
https://twitter.com/InteriorKE/status/1633861616931569665