Kinara wa muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga ametangaza kuwa muungano huo utawaongoza wafuasi wake katika maandamano ya kitaifa, ili kuishinikiza serikali kushughulikia ongezeko la gharama ya Maisha Pamoja na kuondoa ushuru wa juu unaowaumiza wananchi wa kawaida.

Akizungumza Akizungumza jijini Nairobi adhuhuri ya leo baada ya kukamilika kwa makataa ya siku 14 aliyotoa kwa serikali kupunguza gharama ya maisha, Odinga amesema kuwa utawala wa rais Ruto umeshindwa kutimiza ahadi zake na kuwaomba wakenya kujitokeza na kupinga uongozi wa sasa.

Odinga aliyeandamana na viongozi wengine wa muungano huo ameahidi kuandaa maandamano hayo Jumatatu ya tarehe 20 mwezi huu.

March 9, 2023