BY ISAYA BURUGU,10TH MARCH,2023-Waziri wa usalama wa ndani  Prof Kithure Kindiki  amemwagiza mkurugenzi mkuu wa upelelezi wa jinai Mohamed Amin kuharakisha uchunguzi kuhusu kilichopelekea kifo cha kutatanisha cha  Geoffrey Mwathi akiwa katika nyumba ya  mwanamuziki wa benga wa nyimbo za Agikuyu  DJ Fatxo’ mtaani Kasarani  mwezi jana.

Kwenye taarifa Waziri  Kindiki amemuagiza mkuu huyo wa DCI  kuwahusiha watalamu wakuchunguza vifo tatanishi  kusaidia kutatua kesi hiyo .

Mraehemu  Jeff Mwathi/Picha -Hisani

 

DCI wamedhibitisha kuanza uchunguzi wa kisa hicho.

Mnamo tarehe 22 mwezi jana katika nyumba ya makaazi ya Redwood iliyoko karibu na Safaripark Mwathi wenye umri wa miaka 23 alinaswa kwenye  kamera ya CCTV akianguka kutoka Orofa ya kumi  kupitia dirisha  la nyumba hiyo ya kukodi ya DJ FATXO ambaye jina lake halisi ni  Lawrence Njuguna.

 

 

 

 

 

 

March 10, 2023